Hadith · 5821 · KiswahiliSource ↗
Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu - Hadith Translation
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwapige vijakazi wa Mwenyezi Mungu" Akaja Omari kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hivi sasa wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, basi akaruhusu kuwapiga, baada ya muda wakaanza kuzunguka katika familia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu".
- Narrated by
- Imepokelewa na Abu Daud na Ibn Majah
- Grade
- Sahihi
Original Arabic text
لقد طاف بآل محمد نساء كثير يشكون أزواجهن، ليس أولئك بخياركم
عَنْ إِيَاسِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي ذُبَابٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَضْرِبُوا إِمَاءَ اللَّهِ» فَجَاءَ عُمَرُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: ذَئِرْنَ النِّسَاءُ عَلَى أَزْوَاجِهِنَّ، فَرَخَّصَ فِي ضَرْبِهِنَّ، فَأَطَافَ بِآلِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَقَدْ طَافَ بِآلِ مُحَمَّدٍ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ، لَيْسَ أُولَئِكَ بِخِيَارِكُمْ».
رواه أبو داود وابن ماجه · صحيح
النص العربي والتخريج وجميع الترجمات